Taji la Europa League likionyeshwa leo wakati wa droo ya Robo Fainali iliyopangwa makao makuu ya UEFA mjini Nyon, Uswisi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
WASHIKA Bunduki wa London, Arsenal watasafiri kwenda Urusi kumenyana na CSKA Moscow katika Robo Fainali ya Europa League.
The Gunners inapewa nafasi ya kuwatoa wapizani wao hao, lakini tatizo litakuwa ni hawataweza kusafiri na mashabiki kutokana na mgogoro wa kisiasa baina ya nchi hizo mbili.
Katika droo ya Robo Fainali iliyopangwa makao makuu ya UEFA mjini Nyon, Uswisi, mechi zitazikutanisha Atletico Madrid na Sporting Lisbon, RB Leipzig na Marseille na Lazio itamenyana na Salzburg.
Arsenal itakuwa mwenyeji wa klabu ya Urusi Uwanja wa Emirates Alhamisi ya Aprili 5 kabla ya kurudiana Aprili 12, lakini mechi hiyo inaweza kuchezwa chini ya uangalizi kutokana na mgogoro wa kisiasa unaoendelea baina ya nchi hizo mbili.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ameishutumu Urusi kumshambulia mpepelezi Sergei Skripal na binti yake, Yulia Skripal naye akajibu kwa kuwafukuza wanadiplomasia wake 23 waliokuwa mji wa Salisbury aliowatuhumu kuwa ni wapepelezi pia
0 comments:
Post a Comment