Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Singida United imemsimamisha kwa muda usiojulikana mshambuliaji wake raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kambale Salita Gentil (pichani kulia) kwa utivu wa nidhamu.
Taarifa ya Singida United kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba kwa utovu nidhamu alioufanya Kambale jana kawenye mchezo wa hatua ya 32 Bora michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) anasimamishwa mara moja.
Kambale alimpiga ngumi mchezaji wa Green Warriors kipindi cha kwanza na kutolewa kwa kadi nyekundu, hivyo kuiachia mzigo timu wa kucheza pungufu katika sehemu kubwa ya mchezo.
Hata hivyo, Singida United ilishinda kwa penalti 4-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 na kusonga mbele hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo.

0 comments:
Post a Comment