Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco hatakuwemo kwenye msafara wa timu utakaoondoka kesho jioni kwenda Djibouti City kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Gendarmerie Tnare Jumanne.
Bocco aliumia Alhamisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mwadui FC uliomalizika kwa sare ya 2-2 Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Bocco aliifungia Simba bao la kuongoza dakika ya tisa kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Shiza Kichuya baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Iddy Mobby nje kidogo ya boksi.
Lakini dakika ya 29 Bocco akatolewa nje baada ya kumia na mwishoni mwa mchezo timu hizo zikamaliza kwa kufungana mabao 2-2, bao la pili la Simba likifungwa na Mganda, Emmanuel Okwi wakati mabao ya Mwadui FC yalifungwa na beki David Luhende na mshambuliaji, Paul Nonga.
Na baada ya vipimo alivyofanyiwa mjini Dar es Salaam, imeonekana mshambuliaji huyo aliye katika msimu wake wa kwanza Msimbazi tangu awasili Julai mwaka jana kutoka Azam FC hataweza kusafiri kesho.
Baada ya ushindi mnono wa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Jumapili, Simba itakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano Jumanne ugenini.
Na kikosi kitaondoka kesho jioni lakini bila Nahodha wake, Bocco pamoja na wachezaji wengine, wakiwemo kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo ambao hawakuwepo mazoezini leo.
NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco hatakuwemo kwenye msafara wa timu utakaoondoka kesho jioni kwenda Djibouti City kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Gendarmerie Tnare Jumanne.
Bocco aliumia Alhamisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mwadui FC uliomalizika kwa sare ya 2-2 Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Bocco aliifungia Simba bao la kuongoza dakika ya tisa kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Shiza Kichuya baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Iddy Mobby nje kidogo ya boksi.
John Bocco aliyebebwa mgongoni (kulia) hatasafiri kesho kwenda Djibouti |
Na baada ya vipimo alivyofanyiwa mjini Dar es Salaam, imeonekana mshambuliaji huyo aliye katika msimu wake wa kwanza Msimbazi tangu awasili Julai mwaka jana kutoka Azam FC hataweza kusafiri kesho.
Baada ya ushindi mnono wa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika, Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Jumapili, Simba itakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano Jumanne ugenini.
Na kikosi kitaondoka kesho jioni lakini bila Nahodha wake, Bocco pamoja na wachezaji wengine, wakiwemo kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo ambao hawakuwepo mazoezini leo.
0 comments:
Post a Comment