MSHAMBULIAJI Neymar yuko shakani kuichezea Paris Saint-Germain katika mechi ya marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid baada ya Mbrazil huyo kuvunjika mfupa katika mguu wake na kumsababishia maumivu ya kifundo cha mguu.
Katika ushindi wa PSG dhidi ya wapinzani wao, Marseille Jumapili, mwanasoka huyo ghali zaidi duniani aliondoka uwanjani akibubujikwa machozi baada ya kugongana na Bouna Sarr.
Amekwenda kufanyiwa vipimo baada ya mchezo huo walioshinda 3-0 Le Classique na vigogo wa Ligue 1 sasa wamethibitisha kwamba nyota huyo Mbrazil amumia kifundo cha mguu wake wa kulia.
Neymar yuko shakani kuichezea Paris Saint-Germain katika mechi dhidi ya Real Madrid baada ya kuumia 'enka' PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Maumivu hayo yanamaanisha Neymar sasa ataukosa mchezo huo wa marudiano wa PSG iliyofungwa 3-1 kwenye mechi ya kwanza na kikosi cha Unai Emery kitahitaji ushindi wa 2-0 kwenda Robo Fainali.
Vigogo hao wa Ufaransa pia wanahofia kumkosa bekji Mbrazil, Marquinhos baada ya naye kuelezwa pia ameumia.
Bahati nzuri kwa PSG, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alihitaji siku chache cha mapumziko na anatarajiwa kucheza mechi ya marudiano na Madrid.
Pamoja na kukabiliwa na majeruhi hao, PSG walidhihirisha ubora wao dhidi ya mahasimu wao, Marseille Uwanja wa Parc des Princes Jumapili.
Kylian Mbappe, Rolando na Edinson Cavani wote walifunga kikosi cha Emery kikipaa kileleni kwa pointi 16 zaidi ya mahasimu wao, Marseille walio nafasi ya tatu.
0 comments:
Post a Comment