Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya Simba SC na Stand United ya Shinyanga uliopangwa kufanyika Machi 4, mwaka huu umerudishwa nyuma kwa siku mbili maana yae utachezwa Ijumaa wiki hii.
Bodi ya Ligi imeamua kuurudisha nyuma mchezo huo wa nyumbani wa Simba, ili kuwapa fursa pana ya kujiandaa na mchezo wao wa Raundi ya Kwanza Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya El Masry ya Misri.
Mabadiliko hayo yamegusa pia mechi kati ya Lipuli dhidi ya Ndanda FC ambayo nayo imesogezwa mbele hadi Machi 4, badala ya Mach 2 ya awali.
Wachezaji wa Simba, Erasto Nyoni (kushoto) na Mghana, James Kotei (kulia)
Mechi nyingine ni Kagera Sugar dhidi ya Mwadui FC ambayo ilipangwa kufanyika Mach 11, sasa imepelekwa mbele hadi Machi na baada ya hapo, Ligi Kuu itakwenda mapumzikoni tena hadi Machi 22, ili kupisha mechi za kirafiki za kimataifa zilizo katika kalenda ya FIFA.
Ikumbukwe, Bodi ya Ligi pia imeahirisha mchezo mwingine wa Ligi Kuu kati ya Mtibwa Sugar na Yanga SC ya Dar es Salaam uliopangwa kufanyika Machi 3, mwaka huu Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro umeahirishwa.
Sababu za kuuahirisha mchezo huo namba 170 ni kuipa Yanga nafasi nzuri ya maandalizi ya mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers ya Botswana Machi 6 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati Yanga wataikaribishaTownship Rollers ya Botswana Jumanne ya wiki ijayo, Simba SC watakuwa weneyji wa El Masry Jumatano wikiijayo, mechi zote zikichzwa wa Raifa, D res Salaam.

0 comments:
Post a Comment