Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Simba SC inatarajiwa kuwa na kazi nyepesi leo mjini Djibouti City itakapomenyana na wenyeji, Gendarmerie Tnare katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika.
Wepesi huo unatokana na ushindi wa 4-0 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Jumapili ya wiki iliyopita.
Simba SC iliwasili Djibouti Jumapili usiku na jana ikafanya mazoezi yake ya mwisho kuelekea mchezo wa leo, ambao wanatarajiwa kutunisha ushindi wao kutoka 4-0 za kwanza.
Mfungaji wa mabao mawili katika mechi ya kwanza, Nahodha John Raphael Bocco ambaye awali ilielezwa hatakuwemo kwenye safari, ameongozana na timu na pamoja na kutoka kwenye maumivu anaweza kupewa nafasi ya kucheza leo.
Kocha Mfaransa wa Simba SC, Pierre Lechantre (kushoto) akiwa na mmoja wa wasaidizi wake, Mtunisia Mohamed Aymen Hbibi
Bocco aliumia Alhamisi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mwadui FC uliomalizika kwa sare ya 2-2 Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Bocco aliifungia Simba bao la kuongoza dakika ya tisa kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu, uliopigwa na Shiza Kichuya baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Iddy Mobby nje kidogo ya boksi.
Lakini dakika ya 29 Bocco akatolewa nje baada ya kumia na mwishoni mwa mchezo timu hizo zikamaliza kwa kufungana mabao 2-2, bao la pili la Simba likifungwa na Mganda, Emmanuel Okwi wakati mabao ya Mwadui FC yalifungwa na beki David Luhende na mshambuliaji, Paul Nonga.
Ikifanikiwa kumalizia vizuri mchezo wa leo na kuvuka, Simba SC ya kocha Mfaransa Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma, Mtunisia Mohamed Aymen Hbibi ambaye ni mchua misuli na Muharami Mohamed, kocha wa makipa itakutana na mshindi kati ya El Masry ya Misri na Green Buffaloes ya Zambia. Mchezo wa kwanza El Masry ilishindia 4-0 mjini Cairo.
Kila la heri Simba SC katika mchezo wa leo. Tunawatakia ushindi mwingine mnono.
Mfungaji wa mabao mawili katika mechi ya kwanza, Nahodha John Bocco (kulia) ameongozana na timu Djibouti
MARUDIANO MCHUJO KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Jumanne Februari 20, 2018
Masters Security (Malawi) vs Petro Atletico (Angola) (0-5)
Cape Town City (Afrika Kusini) vs Young Buffaloes (Swaziland) (1-0)
Hafia (Guinea) vs Energie (Benin) (0-1)
Anse Reunion (Shelisheli) vs APR (Rwanda) (0-4)
Port Louis (Mauritius) vs Ngazi Sport (Comoros) (1-1)
Deportivo Niefang (Equatorial Guinea) vs New Stars (Cameroon) (1-2)
CS la Mancha (Kongo) vs Tanda (Ivory Coast) (0-0)
CR Belouizdad (Algeria) vs Onze Createurs (Mali) (1-1)
Green Buffaloes (Zambia) vs El Masry (Misri) (0-4)
Gendarmerie (Djibouti) vs Simba (Tanzania) (0-4)
Jumatano Februari 21, 2018
Jwaneng (Botswana) vs Costa do Sol (Msumbiji) (0-1)
FOSA Juniors (Madagascar) vs AFC Leopards (Kenya) (1-1)
Maniema Union (DRC) vs Mangasport (Gabon) (1-0)
Etoile Filante (Burkina Faso) vs Olympic Star (Burundi) (0-0)
Hawks (Gambia) vs Akwa United (Nigeria) (2-1)
Sahel (Niger) vs Al Ittihad (Libya) (0-1)
CARA (Kongo) vs Asante Kotoko (Ghana) (0-1)
Mbour Petite Cote (Senegal) vs RS Berkane (Morocco) (1-2)
Nouadhibou (Mauritania) vs Africa Sports (Ivory Coast) (1-1)
Wolaitta Dicha (Ethiopia) vs Zimamoto (Zanzibar) (1-1)

0 comments:
Post a Comment