// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, February 27, 2018

    CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MAREFA wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa(CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Fosa Juniors ya Madagascar na As Port Louis ya Mauritius utakaochezwa Machi 18,2018 Madagascar.
    Waamuzi walioteuliwa ni mwamuzi wa kati kati Elly Ally Sassii atakayesaidiana na Ferdinand Chacha mwamuzi msaidizi namba moja na Alli Kinduli mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Alphonce Mwandembwa na kamishna wa mchezo huo anatoka Seychelles, Lewis Blaze Madeleine
    Wakati huo Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF Ahmed Msafiri Mgoyi ameteuliwa kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Club Desportivo Costa Do Sol ya Msumbuji na Cape Town City ya Africa Kusini utakaochezwa Machi 7, 2018 Estadio Nacional Dol Zimpeto,Maputo
    Naye Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura ameteuliwa kusimamia mchezo wa Ligi ya mabingwa Africa kati ya Zesco ya Zambia na Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Machi 7,2018 Uwanja wa Levy Mwanawasa uliopo Ndola.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CAF YATAJA WATANZANI SITA KUCHEZESHA NA KUSIMAMIA MECHI LIGI YA MABINGWA NA KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top