TIMU ya taifa ya Zambia imeiadhibu Uganda kwa kuichapa mabao 3-1 katika mchezo wa Kundi B usiku wa jana Uwanja wa Marrakech.
Ushindi huo ni mwendelezo wa ubabe wa Chipolopolo kwa Korongo wa Kampala kwenye fainali za michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya miaka miwili iliyopita pia Zambia kuifunga Uganda 1-0 katika hatua kama hiyo mjini Kigali.
Licha ya Uganda kuuanza vizuri mchezo, lakini walikuwa ni Zambia waliopata bao la kwanza dakika ya 38 kupitia kwa Lazarous Kambole, aliyemtangua kipa kipa wa The Cranes, Benjamin Ochan baada ya pasi ya Ernest Mbewe.
Alex Ng'onga wa Zambia akimuacha chini mchezaji wa Uganda jana Uwanja wa Marakech
The Cranes wakasawazisha bao hilo kwa namna yake dakika mbili baadaye kupitia Derrick Nsibambi kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Zambia, Toaster Nsabata.
Kipindi cha pili kilikuwa ni cha Zambia na wakafanikiwa kupata mabao mawili zaidi, la kwanza akifunga Augustine Mulenga dakika ya 63 akimalizia pasi ya Kambole na Fackson Kapumbu dakika ya 71 kwa shuti la mpira wa adhabu.
Ushindi huo, unawapeleka Chipolopolo kileleni mwa Kundi B, mbele ya Namibia ambao jana waliifunga Ivory Coast 1-0 katika mchezo uliotangulia wa Kundi B, bao pekee la Vetunuavi Charles Hambira dakika ya 90 na ushei.
Mapema mchana katika mchezo uliotangulia wa Kundi, Sudan iliifunga 2-1 Guinea Uwanja wa Mohamed V mjini Casablanca. Mabao ya Sudan yalifungwa na 19' Omer Koko dakika ya 19 na 75' Saifeldin Bakhit dakika ya 75, wakati la Guinea lilifungwa na Sekou Ahmed Camara dakika ya 55.

0 comments:
Post a Comment