// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA YAPEWA IHEFU YA MBEYA, AZAM FC YAPELEKWA MOROGORO KWA SHUPAVU FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA YAPEWA IHEFU YA MBEYA, AZAM FC YAPELEKWA MOROGORO KWA SHUPAVU FC - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

        Friday, January 05, 2018

        YANGA YAPEWA IHEFU YA MBEYA, AZAM FC YAPELEKWA MOROGORO KWA SHUPAVU FC

        Na Salma Suleiman, DAR ES SALAAM
        VIGOGO Azam FC na Yanga SC watasafiri kwenda mikoani kumenyana na timu za Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
        Yanga SC watakwenda Mbeya kuifuata Ihefu, mechi itakayopigwa Uwanja wa Sokoine mjini humo, wakati Azam FC watakwenda Uwanja wa CCM Mkamba mkoani Morogoro kumenyana na Shupavu FC.  
        Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
        Timu ya kocha Freddy Felix Minziro, KMC itakuwa mwenyeji wa Toto mjini Dar es Salaam, wakati Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. 
        Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
        Mechi nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga. 
        Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. 
        Mechi zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.

        MECHI ZOTE HATUA YA 32 BORA
        KMC V Toto Africans 
        Maji Maji v Ruvu Shooting
        Njombe Mji v Rhino Rangers
        Kiluvya Utd v JKT Oljoro
        Ndanda Fc v Biashara United
        Pamba SC v Stand United
        Polisi TZ v Friends Rangers
        JKT Tanzania v Polisi Dar
        Ihefu FC v Yanga SC
        Mwadui FC v Dodoma FC 
        Green Warriors v Singida United
        Tanzania Prisons v Burkina Faso
        Kariakoo United v Mbao FC
        Maji Maji Rangers Lindi v Mtibwa Sugar
        Kagera Sugar v Buseresere FC 
        Shupavu FC v Azam FC
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: YANGA YAPEWA IHEFU YA MBEYA, AZAM FC YAPELEKWA MOROGORO KWA SHUPAVU FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry