Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MECHI za Hatua ya 32 Bora Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) zinatarajiwa kuanza leo kwa vigogo, Azam na Yanga kujitupa viwanjani baada ya wakubwa wenzao, Simba kutolewa mapema.
Zote Azam FC na Yanga SC zimesafiri hadi mikoani kumenyana na timu za Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Yanga SC leo watakuwa wageni wa Ihefu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, wakati Azam FC watamenyana na wenyeji, Shupavu FC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Green Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya washindi wa pili wa msimu uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Maji Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mechi nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Tanzania Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mchezo kati ya KMC ya kocha Freddy Felix Minziro wa Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam umeahirishwa hadi Februari 7 wakati mechi nyingine zite zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.

MECHI ZOTE HATUA YA 32 BORA
JANUARI 30, 2018
IHEFU VS YANGA –MBEYA
JKT TZ VS POLISI DAR
POLISI TZ VS FRIEND RANGERS
SHUPAVU FC VS AZAM FC
NDANDA VS BIASHARA
KARIAKOO LINDI VS MBAO
KAGERA SUGAR VS BUSERESERE
JANUARI 31, 2018
MAJIMAJI FC VS RUVU
TZ PRISONS VS BURKINA
KILUVYA VS JKT OLJORO
GREEN WARRS VS SINGIDA UNITED
PAMBA VS STAND UNITED
NJOMBE MJI VS RHINO RANGERS
JANUARI 7, 2018
KMC VS TOTO AFRICANS
0 comments:
Post a Comment