Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WAAMUZI kutoka Sudan Kusini wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Soka Afrika (CAF) kuchezesha mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba ya Tanzania na Gendarmerie Tnale ya Djobouti itakayochezwa Februari 21, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mwamuzi wa kati atakuwa Alier Michael James akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Suleiman Gassim ,mwamuzi msaidizi namba mbili Gasim Madir Dehiya wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Kalisto Gumesi Simon Samson na Kamishna wa mchezo huo kutoka Botswana ni Mmonwagotlhe Edwin Senai.
Nahodha wa Simba SC, John Bocco (kushoto) ataiongoza timu yake dhidi ya Gendarmerie Tnale ya Djobouti Februari 21 Uwanja wa Taifa
Mchezo wa marudiano utakaochezwa Djibouti kati ya Februari 20 na 21,2018 wenyewe utachezeshwa na waamuzi kutoka Burundi na Kamishna wa mchezo atatokea nchini Rwanda.
Mwamuzi wa kati ni Eric Manirakiza akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Pascal Ndimunzigo,mwamuzi msaidizi namba mbili Willy Habimana,mwamuzi wa akiba Pacifique Ndabihawenimana na kamishna Gaspard Kayijuka.

0 comments:
Post a Comment