Robin van Persie amerejea Feyenoord miaka 14 tangu aondoke kuhamia Arsenal PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MSHAMBULIAJI Robin van Persie amekamilisha uhamisho wake kurejea klabu yake ya ujanani, Feyenoord — miaka 14 tangu aondoke Uholanzi kwenda kujiunga Arsenal.
Mshambuliaji huyo Mholanzi alianzia soka katika klabu hiyo, akiibukia kwenye akademi, kabla ya kwenda kufunga mabao 226 kwenye klabu za Arsenal, Manchester United za England na Fenerbahce ya Uturuki.
Lakini alirejea Jumatatu, akisaini mkataba wa miezi 18 baada ya Fenerbahce kukubali kumuachia aondoke kama mchezaji huru mwezi huu.
Baada ya kushindwa kung'ara nchini Uturuki, Van Persie alikubali kurejea nyumbani Ijumaa alipowasili na leo kukamilisha uhamisho wake.
Baada ya kurejea, Van Persie sasa atakuwa anavaa jezi namba 32 msimu huu, akirejea kwenye namba yake ya kwanza aliyovaa wakati anaibuka mwaka 2002.
0 comments:
Post a Comment