Ryan Giggs ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Wales, Ryan Giggs ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Gwiji huyo wa Manchester United amejitosa kwenye soka na uchambuzi tangu astaafu soka, lakini hakuwa kupata ajira rasmi.
Bodi ya nchi hiyo imemtihibitisha Giggs kuwa kocha mpya wa timu hiyo kupitia kwenye Twitter.
Giggs alikuwa mmoja wa makocha wanne waliokuwa wanawania nafasi hiyo ambao walifanyiwa usaili Alhamisi- kocha wa sasa wa Sunderland, Chris Coleman, na mchezaji mwenzake wa zamani wa Wales, Craig Bellamy, Mark Bowen — ambyae ameondoka Stoke — na Msaidizi, Osain Roberts.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 sasa atakuwa na jukumu la kuisaidia timu hiyo kufuzu Euro 2020, baada ya kushindwa kufuzu kwenye fainali za Kombe la Dunia Urusi 2018.
Giggs aliichezea timu yake ya taifa mechi 64 na ninfuraha iliyoje kwake mwishowe anapata nafasi pia kuwa kocha.
0 comments:
Post a Comment