TIMU ya Taifa ya Uganda imetolewa kwenye michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee baada ya kufungwa 1-0, bao pekee la Panduleni Nekundi dakika ya 90 jana na Namibia katika mchezo wa Kundi B uliofanyika Uwanja wa Marrakech nchini Morocco.
Hicho ni kipigo cha pili mfululizo kwa timu hiyo inayofundishwa na kocha Mfaransa, Sebastien Desabre tangu Desemba mwaka jana baada ya kufungwa 3-1 na Zambia katika mchezo wa kwanza Januari 14.
Kwa ushindi wake, Namibia inaungana na Zambia iliyoshinda 2-0 dhidi ya Ivory Coast leo, mabao ya Augustine Mulenga dakika za nane na 73 hapo hapo Uwanja wa Marrakech.
Uganda sasa itateremka uwanjani tena Jumatatu kumenyana na Ivory Coast kukamilisha mechi zake za Kundi hilo kabla ya kurejea Kampala.

0 comments:
Post a Comment