Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
HATUA ya 32 Bora ya michuano ya Azam Sports Federetion Cup (ASFC) inaendelea leo kwa mechi sita zaidi kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini, Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, Maji Maji Rangers wakiikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Ilulu itashuhudia mchezo wa pili mfululizo wa ASFC timu za Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara zikiendelea kumenyana na timu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya jana Kariakoo United kutolewa na Mbao FC.
Uwanja wa Maji Maji mjini Songea wenyeji, Maji Maji FC watawakaribisha Ruvu Shooting ya Pwani, Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Tanzania Prisons watawakaribisha na Burkina Faso ya Morogoro na Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, Kiluvya United watakuwa wenyeji wa JKT Oljoro.
Mtibwa Sugar ya Morogoro wapo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi leo kuwakabili wenyeji, Maji Maji Rangers
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Green Warriors waliowatoa waliokuwa mabingwa watetezi, Simba kwenye hatua iliyotangulia, wataikaribisha Singida United, Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Pamba ‘TP Lindanda’ watakuwa wenyeji wa Stand United ya Shinyanga na Uwanja wa Saba Saba mjini Njombe, wenyeji Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers ya Tabora.
Mchezo kati ya KMC na Toto Africans umesogezwa mbele hadi Januari 7 uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Ikumbukwe katika mechi za jana, Azam FC iliwatoa wenyeji Shupavu FC kuwa kuwachapa mabao 5-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Yanga iliwatoa wenyeji Ihefu kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Ndanda FC ilishinda kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 na Biashara United ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Mechi nyingine ASFC; Mbao FC ilisshinda 1-0 dhidi ya wenyeji Kariakoo United Uwanja wa Ilulu, Lindi, Dodoma FC ilishinda 2-1 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Buseresere FC ilishinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Polisi Tanzania iliifunga Friends Rangers 2-1 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi na JKT Tanzania iliifunga Polisi Dar 1-0 mjini Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment