MASHABIKI waliosafiri walilazimika kuondoka jukwaani kuvamia uwanjani wakati mchezo wa Ligi Kuu ya Ureno, maarufu kama Primeira Liga kati ya Porto na Estoril ukivunjika.
Hiyo ilifuatia mashabiki hao kugundua nyufa zenye mipasuko mikubwa katika jukwaa la Uwanja wa Antonio Coimbra da Mota na kuondoka kunusuru maisha yao kwa kuhofia jukwaa huilo kudondoka.
Wenyeji walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0 hadi mapumziko, lakini makocha wenye heshima walikubali kufanya mazungumzo, kundi la mashabiki wa timu ngeni likaagizwa na walinzi kuingia kwa mujibu wa gazeti la The Daily Record la Scotland.
Mashabiki wakiondoka jukwaani kuelekea jukwaani baada ya kuona nyufa kwenye Uwanja wa Antonio Coimbra da Mota jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Uamuzi huo ulichukuliwa na walinzi waliothibitisha jukwaa hilo halikuwa salama baada ya mashabiki hao kusema waliona nyufa wakati wanakwenda chooni na mipasuko mingine mikubwa ukutani.
Kiasi cha mashabiki 2,500 wa Porto wamesafiri kwenda Estoril wakati Porto wakisaka pointi za kuwarejesha kileleni mwa Primeira Liga ambako kwa sasa wapo Sporting.
Wakati uchunguzi juu ya usalama wa jukwaa hilo ukiendelea, Estoril wanatarajiwa kurejea kuanza kuutumia tena uwanja wao huo wa nyumbani kati ya Januari 30 na Februari 4.
0 comments:
Post a Comment