Na Mwandishi Wetu, DAR ES SWALAAM
KOCHA wa Yanga SC, George Lwandamina leo amewaanzisha pamoja washambuliaji, Mkongwe Mrundi Amissi Tambwe na chipukizi mzawa, Yohanna Nkomola katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viungo wa pembeni katika mchezo wa leo watakuwa Ibrahim Ajib na Pius Buswita wakati katikati watakuwapo Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na mzawa Raphael Daudi.
Safu ya ulinzi itaundwa na kipa Mcameroon, Youthe Rostand, mabeki wazawa watupu Hassan Kessy kulia, Mwinyi Hajji Mngwali kushoto na Andrew Vincent ‘Dante’ na Said Juma ‘Makapu’ katikati.
Ligi Kuu inaendelea leo kwa michezo mitatu, mbali na Yanga kuonyeshana kazi na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, mjini Mbeya Tanzania Prisons wanaikaribisha Azam FC Uwanja wa Sokoine na Mwadui FC ni wenyeji wa Ndanda FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Youthe Rostand, Hassan Kessy Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’, Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daudi, Amissi Tambwe, Yohanna Nkomola na Ibrahim Ajib.
Benchi; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Gardiel Michael, Pato Ngonyani, Juma Mahadhi, Said Mussa ‘Ronaldo’ na Emmanuel Martin.
KOCHA wa Yanga SC, George Lwandamina leo amewaanzisha pamoja washambuliaji, Mkongwe Mrundi Amissi Tambwe na chipukizi mzawa, Yohanna Nkomola katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Viungo wa pembeni katika mchezo wa leo watakuwa Ibrahim Ajib na Pius Buswita wakati katikati watakuwapo Mkongo Papy Kabamba Tshishimbi na mzawa Raphael Daudi.
Safu ya ulinzi itaundwa na kipa Mcameroon, Youthe Rostand, mabeki wazawa watupu Hassan Kessy kulia, Mwinyi Hajji Mngwali kushoto na Andrew Vincent ‘Dante’ na Said Juma ‘Makapu’ katikati.
Amissi Tambwe (kushoto) ameanzishwa tena na leo katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting |
Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Youthe Rostand, Hassan Kessy Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’, Said Juma ‘Makapu’, Papy Kabamba Tshishimbi, Pius Buswita, Raphael Daudi, Amissi Tambwe, Yohanna Nkomola na Ibrahim Ajib.
Benchi; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Gardiel Michael, Pato Ngonyani, Juma Mahadhi, Said Mussa ‘Ronaldo’ na Emmanuel Martin.
0 comments:
Post a Comment