KLABU ya Arsenal imekubali kufanya usajili wa rekodi katika historia yake, kutoa Pauni Milioni 55.4 kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang.
Nyota huyo wa Gabon, ambaye amekuwa akitakiwa na The Gunners kwa mwezi wote huu, pia anatarajiwa kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu hiyo.
Arsenal imempa ofa ya mkataba wa miaka mitatu na nusu Aubameyang kwa mshahara wa Pauni 180,000 kwa wiki.
Wakati huo huo, gazeti la BILD limeripoti kwamba Borussia Dortmund linamtaka mshambuliaji wa Chelsea, Michy Batshuayi kwa mkopo ahamie Bundesliga kuziba pengo la Aubameyang.
Arsenal imekubali kutoa Pauni Milioni 55.4 kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Dortmund ilitaka kumsajili Giroud, lakini ikasitisha mpango wa kumchukua Mfaransa huyo baada ya mchezaji huyo kusema anataka kubaki England.
Sasa Aubameyang akienda Arsenal, Giroud atahamia Chelsea kama wapinzani wao wa London watafika bei ya Pauni Milioni 35.
Chelsea ilimjadili Giroud mwishoni mwa wiki baada ya kuona wanasotea saini ya wachezaji wa Roma, Edin Dzeko na Emerson Palmieri.
Arsene Wenger, ambaye anataka kuunda kikosi imara Arsenal ambacho kitaingia tena kwenye Ligi ya Mabingwa na amepigwa picha mapema leo akiingia Uwanja wa mazoezi wa timu hiyo.
Wenger kwa sasa anaiandaa Arsenal kwa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea City kesho Uwanja wa Liberty.
0 comments:
Post a Comment