// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARISTICA CIOABA ASEMA MECHI YAO NA YANGA ITAKUWA NGUMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARISTICA CIOABA ASEMA MECHI YAO NA YANGA ITAKUWA NGUMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, January 23, 2018

    ARISTICA CIOABA ASEMA MECHI YAO NA YANGA ITAKUWA NGUMU

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba amesema mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga utakuwa mgumu na watacheza kwa umakini ili waibuke na ushindi.
    Azam FC watakuwa wenyeji wa Yanga SC Jumamosi wiki hii Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakitoka kushinda 2-0 ugenini dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumapili.
    Cioaba amesema Yanga ni moja ya timu kubwa nchini ikitoka kutwaa ubingwa wa ligi msimu uliopita na kudai kuwa wataingia uwanjani na kuonyesha umakini mkubwa.
    Kocha Aristica Cioaba amesema mechi na Yanga itakuwa mgumu Jumamosi Chamazi

    “Mechi itakuwa Chamazi, hautakuwa mchezo mwepesi nitakuwa na muda wa siku tatu wa maandalizi kwa kuwa nina safari ndefu sana na wachezaji wanauchovu kidogo lakini siku hizo tatu nitawaunganisha vema wachezaji na kujaribukufanya vizuri dhidi ya Yanga Chamazi, sihitaji kupoteza mchezo wowote hapo baadaye,”amesema.
    Hadi sasa ikiwa imecheza mechi 14 za ligi, Azam FC imefanikiwa kuwa rekodi bora baada ya kutopoteza mchezo hata mmoja, ikiwa imeshinda mechi nane na sare sita ikiwa kileleni kwa pointi zake 30 ikiizidi mechi moja Simba ambayo ipo nafasi ya pili ikijikusanyia 29.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARISTICA CIOABA ASEMA MECHI YAO NA YANGA ITAKUWA NGUMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top