Manchester United imetangaza kumsajili mshambuliaji Alexis Sanchez kutoka Arsenal, zote za England PICHA ZAIDI GONGA HAPA
KLABU ya Manchester United imekamilisha uhamisho wa mshambuliaji Alexis Sanchez kwa mkataba wa miaka minne na nusu kutoka Arsenal na Henrikh Mkhitaryan anakwenda upande wa pili.
Akiuzungumzia uhamisho wake, Alexis Sanchez amesema: "Nina furaha kujiunga na klabu kubwa duniani. Nimekuwa Arsenal kwa miaka mitatu na nusu mizuri na imenipa kumbukumbu nzuri klabu hiyo kubwa na mashabiki wake.
"Nafasi ya kucheza kwenye Uwanja huu wa kihistoria na kufanya kazi na Jose Mourinho ni ambayo nisingeweza kuikataa. Ninayo furaha kuwa mchezaji wa kwanza wa Chile kuchezea timu ya kwanza ya United na ninatumai ninaweza kuwaonyesha mashabiki wetu dunia nzima kwa nini klabu imenileta hapa,".
Jose Mourinho kwa upande wake amesema: "Alexis ni mmoja wa washambuliaji bora duniani na tutakamilisha safu yetu ya ushambuliaji ya wachezaji chipukizi na wenye vipaji. Ataleta matarajio yake, dhamira na haiba, sifa ambazo zimemfanya awe mchezaji wa Manchester United na mchezaji ambaye anaifanya timu iwe madhubuti na mashabiki wajivunie timu yao,".
"Ningependa kumtakia kila la heri Henrikh, mafanikio yote na furaha ambayo nina uhakika anakwenda kuipata. Ni mchezaji ambaye hatutamsahau, hususan kutokana na mchangi wake kwenye ushindi wa taji letu la Europa League,"amesema.
0 comments:
Post a Comment