// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ZANZIBAR HEROES YAWAONYESHA NJIA YA KURUDIA NYUMBANI KILIMANJARO STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ZANZIBAR HEROES YAWAONYESHA NJIA YA KURUDIA NYUMBANI KILIMANJARO STARS - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, December 07, 2017

    ZANZIBAR HEROES YAWAONYESHA NJIA YA KURUDIA NYUMBANI KILIMANJARO STARS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    ZANZIBAR imeendeleza ‘umwamba’ katika michuano ya CECAFA Challenge baada ya mchana huu kuwachapa ndugu zao, Tanzania Bara mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi A uliofanyika Uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya.
    Huo unakuwa ushindi wa pili kwa timu ya kocha Hemed Moroccco baada ya juzi kuichapa Rwanda 3-1 katika mchezo wake wa kwanza na sasa Zanzibar Heroes wanaongeza matumaini ya kwenda Nusu Fainali.   
    Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdul Karim wa Rwanda, aliyesaidiwa na Tigle Belachew wa Ethiopia na Iterve kakunze wa Burundi, Tanzania Bara walikwenda kupumzika wakiwa wanaongoza kwa baop 1-0.
    Kiungo Mohammed Issa 'Banka' wa Zanzibar akimtoka Shiza Kichuya wa Tanzania Bara 

    Hamad Makame wa Zanzibar Heroes akikabiliana na mshambuliaji wa Serengeti Boys, Elias Maguri 

    Bao hilo lilifungwa na Nahodha, kiungo Himid Mao Mkami dakika ya 28 akifumua shuti ndani ya  boksi baada ya pasi ya Daniel Lyanga kufuatia wawili hao kugongeana.
    Mapema dakika ya tisa Kilimanjaro Stars ilipata pigo baada ya beki wake wa kati, Kevin Yondan kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na beki wa pembeni, Boniphace Maganga.
    Baada ya Maganga kuingia akaenda kucheza beki ya kulia na Erasto Nyoni akaingia ndani kucheza pamoja na Kennedy Wilson Juma beki ya kati.
    Kipindi cha pili, Zanzibar Heroes waliongeza kasi ya mashambulizi hadi wakafanikiwa kupata bao la kusawazisha, lililofungwa na Kassim Suleiman Khamis dakika ya 66 aliyemlamba chenga beki Boniphace Maganga na kuingia ndani ya boksi kabla ya kufumua shuti kutokea pembezoni mwa Uwanja kushoto ambalo lilimpita kipa Aishi Manula.
    Wakati Tanzania Bara wakijaribu kutafuta bao la pili, wakajikuta wanafungwa wao kwa shambulizi la kushitukizwa baada ya kiungo mkongwe, Kassim Suleiman ‘Selembe’ kumlamba chenga Maganga na kutia krosi iliyounganishwa nyavuni na Ibrahim Hamad Ahmada dakika ya 78.
    Zanzibar Heroes wakapata pigo dakika ya 86 baada ya mfungaji wake wa bao la kusawazisha, Khamis kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Ibrahim Abdallah Hamad.
    Tanzania Bara sasa watahitaji lazima ushindi dhidi ya Kenya na Rwanda ili kuangalia uwezekano wa kwenda Nusu Fainali, jambo ambalo hakika ni gumu.
    Kikosi cha Tanzania Bara kilikuwa; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Kennedy Wilson, Kevin Yondan/Boniphace Maganga dk9, Hamisi Abdallah/Jonas Mkude dk73, Himid Mao, Muzamil Yassin, Elias Maguli/Yahya Zayed dk76, Daniel Lyanga na Shiza Kichuya.
    Zanzibar; Mohammed Abdulrahman, Ibrahim Mohammed Said, Mwinyi Hajji Mngwali, Abdallah Salum Kheri, Issa Haidar Dau, Abdulaziz Makame Hassan, Mohammed Issa ‘Banka’, Mudathir Yahya/Kassim Suleiman Khamis dk58/Ibrahim Abdallah Hamad dk87, Ibrahim Hamad, Feisal Salum Abdallah na Hamad Mshamata Makame.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZANZIBAR HEROES YAWAONYESHA NJIA YA KURUDIA NYUMBANI KILIMANJARO STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top