Na Mwandishi Wetu, MACHAKOS
NDUGU, Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ wanakutana leo Uwanja wa Jomo Kenyatta mjini Machakos kuanzia Saa 8.00 mchana katika mchezo wa Kundi A Kombe la CECAFA Challenge.
Mchezo huo unatarajiwa kushuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Pindi Hazara Chana ambaye anaiwakilisha nchi katika Kenya.
Zote Kilimanjaro Stars ya kocha Kocha mkuu Ammy Ninje na Zanzibar Heroes ya Hemed Morocco jana asubuhi zimefanya mazoezi yao ya mwisho kwenye Uwanja wa Machakos Academy kujiandaa na mchezo wa leo.
Kocha Ninje amesema maandalizi ya mchezo huo dhidi ya Zanzibar yamekamilika na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Libya.
Mshambuliaji wa Tanzania Bara, Ibrahim Ajib akiruka juu mazoezini jana. Je, leo atawazima Zanzibar?
Mbaraka Yusuph ndio mchezaji pekee atakayekosekana kutokana na kusumbuliwa na mejeraha ya misuli lakini Kocha Ninje amesema ana washambuliaji wanne ambao atawatumia kuziba nafasi hiyo ya Mbarak.
Nahodha Himid Mao amesema mechi hiyo itakuwa ngumu lakini wako tayari kupambana kupata matokeo ya ushindi kwakuwa kila mmoja wao ana morali kubwa na nia ya kupata ushindi.
Amesema kikubwa watatakiwa kutulia na akili zao kuzielekeza uwanjani kuhakikisha Kilimanajro Stars inabeba pointi zote 3.
Kwa upande wakem Morocco amesema hana wasiwasi Kilimanjaro Stars ni timu ambayo anaifahamu vizuri na wachezaji wanafahamiana pia.
Morocco amesema anatarajia ushindi wa pili mfululizo leo na kujiweka katika mazingira mazuri ya kwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo.
Wakati Kilimanjaro Stars ililazimishwa sare ya 0-0 na Libya katika mchezo wa kwanza Desemba 3, Zanzibar Heroes walishinda 3-1 dhidi ya Rwanda katika mchezo wao wa kwanza juzi.
Kilimanjaro Stars inashuka kwenye mchezo wa kesho ikiwa na pointi moja katika Kundi hilo la A ambalo linaongoza na Kenya wenye pointi 4 wakifuatiwa na Zanzibar wenye pointi 3, Libya wenyewe wana pointi 2 wakati Rwanda wanaburuza mkia wakiwa hawana pointi wakifungwa kwenye michezo yake yote miwili iliyochezwa.
Timu hizo za Kundi A zinaingia Uwanjani hiyo kesho zikiwa kwenye nafasi tofauti wakati Kilimanjaro Stars ikikamata nafasi ya nne ikiwa na pointi moja iliyoipata kwa kutoka suluhu bila kufungana na Libya, Zanzibar Heroes wao wapo kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu baada ya kushinda mechi yake ya kwanza dhidi ya Rwanda.
Timu nyingine kwenye Kundi hilo mbali ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes ni Libya na Rwanda ni wenyeji Kenya “Harambee Stars”. Kundi B lenyewe linacheza mechi zake huko Kakamega likiwa na timu za Uganda, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.

0 comments:
Post a Comment