BONDIA Tyson Fury ameruhusiwa kucheza ngumi za kulipwa baada ya kukubali adhabu yake ya kufungiwa miaka miwili kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu zilizopigwa marufuku michezoni.
Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu duniani, amekuwa nje ya ulingo tangu amshinde Wladimir Klitschko Novemba mwaka 2015.
Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu duniani, amekuwa nje ya ulingo tangu amshinde Wladimir Klitschko Novemba mwaka 2015.
Muingereza huyo alifungiwa Juni mwaka 2016 na taasisi ya Kupambana na Dawa za Kulevya Michezoni nchini Uingereza (UKAD), lakini sasa anaweza kuanza kucheza tena mwakani akikata leseni upya.
0 comments:
Post a Comment