KIUNGO Raheem Sterling anatarajiwa kupewa mkataba mpya mnono Manchester City baada ya kuonyesha kiwango cha juu hivi karibuni.
Sterling amekuwa mchezaji muhimu hivi karibuni Man City akiifungia mabao ya ushindi na kuifanya ishinde mechi mfululizo hadi 13.
Tayari mchezaji huyo wa kimataifa wa England amefunga mabao tisa katika Ligi Kuu ya England msimu huu, na 13 jumla kwenye michuano yote, jambo ambalo linaivutia City kumfanya awe mchezaji ghali zaidi kwa mujibu wa gazeti la The Sun.
Taarifa ziasema klabu hiyo ya Etihad inataka kumpa mchezaji huyo mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki kumfanya Sterling awe mchezaji anayelipwa zaidi katika klabu na Ligi Kuu.
Raheem Sterling anatarajiwa kupewa mkataba mpya mnono Manchester City baada ya kazi nzuri hivi karibuni
Mazungumzo yanayoendelea yatamfanya Sterling akaribie hadhi ya nyota kama Lionel Messi na Neymar kimaslahi.
Ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 atapewa mkataba huo mpya, atampiku nyota wa Manchester United, Paul Pogba.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa, Pogba kwa sasa anaongoza kwa kulipwa Ligi Kuu England akipata Pauni 290,000 kwa wiki.
0 comments:
Post a Comment