Cristiano Ronaldo akiwa ameshika tuzo ya Ballon d'Or baada ya kukabidhiwa leo mjini Paris, Ufaransa PICHA ZAIDI GONGA HAPA
MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, maarufu kama Ballon d'Or mwaka 2017.
Ronaldo ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya tano katika sherehe zilizofanyika ukumbi wa Eiffel Tower akiwaangusha Muargentina Lionel Messi na Mbrazil Neymar.
Ronaldo anayechezea Real Madrid sasa analingana na Messi wa Barcelona, zote za Hispania kwa kutwaa mara nyingi zaidi Ballon d'Or, kila mmoja mara tano.
Na mafanikio yake yanafuatia kuiwezesha Real Madrid kutwaa Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga msimu uliopita wa 2016-17.
Mshindi wa 2017 ametajwa kwa mbwembwe za aina yake, akitokea kwenye video ukumbi wa Eiffel Tower na akaonekana Ronaldo amesimama akiwa ameshika tuzo yake.
"Ndiyo, najisikia furaha. Ni wakati mzuri katika maisha yangu," amesema Ronaldo wakati anakabidhiwa tuzo. Ni kitu fulani natumai kushinda kila mwaka. Nawashukuru wachezaji wenzangu wa Real Madrid. Na ninataka kuwashukuru watu wengine walionisaidia kufikia kiwango bhiki,".
Ronaldo mwenye umri wa miaka 32, ambaye baadaye alifuatwa na mama yake, Maria Dolores dos Santos Aveiro na mtoto wake wa kioume mkubwa, Cristiano Ronaldo Jr huku mpenzi wake, Georgina Rodriguez akitazama kutoka eneo la watu.
Ronaldo ameshinda tuzo hiyo inayoandaliwa nchini Ufaransa baada ya kuwabwaga wachezaji wengine 29 kutokana na kura za kikundi cha Waandishi wa Habari 173.
Messi ameshika nafasi ya pili, kwa mara ya saba wawili hao wakishika nafasi mbili za mwanzo za Ballon d'Or katika ushindani wao na Neymar amekuwa wa tatu.
George Weah anabaki kuwa Mwafrika pekee aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 1995 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
George Weah anabaki kuwa Mwafrika pekee aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 1995 PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment