WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva ameteuliwa kwenye kikosi bora cha mwezi cha Ligi Kuu ya Morocco baada ya kazi nzuri Novemba.
Msuva amefunga mabao mawili na kuseti matatu, Difaa Hassan El Jadida ikishinda mechi tatu na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi ya Morocco, maarufu kama Botola.
Na baada ya mafanikio hayo, si ajabu Msuva anateuliwa kikosi bora cha mwezi Novemba chga Botola.
Msuva ameunza vizuri pia mwezi Desemba baada ya kuifungia bao moja Difaa Hassan El - Jadida ikishinda 4-1 dhidi ya Khouribga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan Jumapili.
Msuva, mshambuliaji wa zamani wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC alifunga bao lake dakika ya 71, likiwa la nne katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Morocco maarufu kama Botola.
Simon Msuva ameunza vizuri pia mwezi Desemba baada ya kuifungia bao moja Difaa Hassan El - Jadida ikishinda 4-1 dhidi ya Khouribga
Mabao mengine matatu ya DHJ siku hiyo yote yalifungwa na mshambuliaji chipukizi Mmorocco, Hamid El Ahadad dakika za 30, 40 na 57.
Na kwa ushindi huo, Difaa Hassan El Jadida imefikisha pointi 17 baada ya kucheza mechi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Botola, nyuma ya Hassania Agadir yenye pointi 19 za mechi 10.
0 comments:
Post a Comment