Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Mbaraka Yusuph, anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kwenda mjini Cape Town, Afrika Kusini kwa uchunguzi wa goti lake la kushoto baada ya kuumiza kiungo ambacho kitaalamu kinajulikana kama meniscus (washa).
Yusuph aliumia akiwa na kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ wakati ikicheza na Libya kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la CECAFA Challenge ulifanyika nchini Kenya Desemba 3 mwaka huu.
Mbara aliyesajiliwa msimu huu kutoka Kagera Sugar ataondoka akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, atakayekuwa akishughulikia taratibu zake zote za matibabu.
Mshambuliaji Mbaraka Yusuph (kulia) akiwa na Kocha Mromania, Aristica Cioaba
Katika hatua nyingine, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amethibitisha timu kupata vibali vya kufanyia kazi nchini vya mshambuliaji wake mpya, Bernard Arthur kutoka Ghana.
Maganga amesema kwamba Arthur sasa ni rasmi ataruhusiwa kucheza kwenye mchezo ujao wa Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) dhidi ya Area C United ya Dodoma utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Jumamosi hii saa 1.00 usiku.
“Bernard Arthur yupo huru kucheza mashindano yote ambayo yanahusu Azam FC kwa maana kwamba taratibu za kupata vibali vyake vya kufanya kazi nchini zimekamilika, sisi Azam FC tunamatumaini kwamba kwa kushirikiana na wenzake atatoa mchango mkubwa na vilevile kuweza kuhakikisha kuwa safu yetu ya ushambuliaji itazidi kuchangamka zaidi,” alisema.
Arthur amesajiliwa akitokea Liberty Professional ya Ghana kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo hadi sasa ameshafunga mabao matatu kwenye mechi za kirafiki alizocheza.
Alifunga la kwanza dhidi ya Friends Rangers katika sare ya bao 1-1 kabla ya kutupia mawili, Azam FC ilivyoilaza Villa Squad mabao 7-1 mechi zote zikichezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment