BINGWA wa dunia wa uzito wa juu, Anthony Joshua amevunja kioo kwa ngumi moja tu mjini Amsterdam, Uholanzi – wakati wa ufunguzi wa duka katika Jiji hilo.
Bingwa huyo wa IBF na WBA amekuwa nje ya ulingo tangu ampige Carlos Takam mwishoni mwa mwezi Oktoba na kufanikiwa kutetea mataji yake aliyoyatwaa kwa kumshinda Wladimir Klitschko mwezi Aprili.
Joshua ametumia muda zaidi wa kuwa Amsterdam Alhamisi kwa kubomoa kioo cha duka jipya linalomilikiwa na Under Armour.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 28 ameposti video yake kwenye akaunti yake ya Instagram akifungua duka hilo.
"Wakati mwingine inahitaji ngumi moja tu," ameandika Joshua maelezo ya picha hiyo. "Najivunia kufungua @underarmour Brand House mjini Amsterdam #IWILL.'
Joshua, ambaye anadhaminiwa na kampuni hiyo ya Marekani, amekuwa bize wiki za karibuni kwa mazungumzo ya pambano ya kuunganisha mataji na Deontay Wilder.
Wilder na Joshua walitarajiwa kutaja tarehe ya pambano lao lao mwakani, lakini inaonekana mambo yatakuwa tofauti baada ya promota Muingereza, Eddie Hearn kukataa.
0 comments:
Post a Comment