MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo atasaidia ujenzi wa hospitali ya watoto mjini Santiago, Chile.
Mchezaji huyo anayelipwa zaidi duniani, Pauni 450,000 kwa wiki, anafahamika kwa uungwana wake katika mambo ya hisani.
Ronaldo ameungana na mfanyabiashara wa Italia, Alessandro Proto kufadhili ujenzi huo unaitakuwa kukamilika mwaka 2020.
Na kuna hospitali zaidi wamepanga kujenga Amerika Kusini. Taarifa isiyo rasmi ya kampuni ya uanasheria ya Brafman & Associates yenye maskani yake New York imesema: "Mwanasoka wa Ureno Cristiano Ronaldo atajenga hospitali ya watoto mjini Santiago, Chile mwaka 2020,".
Cristiano Ronaldo ameungana na mfanyabiashara wa Italia, Alessandro Proto kufadhili ujenzi wa hospitali Chile PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Ronaldo ni Balozi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia watoto, Unicef na Dira ya Dunia na kwa kawaida amekuwa akichangaia taasisi zote hizo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 pia amekuwa akijitolea damu na mifupa tangu mtoto wa kiume wa mchezaji mwenzake wa zamani, Carlos Martins augue saratani ya damu mwaka 2011.
Na wakati mama yake, Dolores Aveiro aliponusurika na saratani ya matiti miaka 10 iliyopita, Ronaldo alichangia Pauni 120,000 zahanati iliyomtibu.
Mshindi huyo wa Ballon d'Or tano, wakati anaendelea kufanya vizuri uwanjani, lakini wema wake nje ya Uwanja nao pia unazidi kumjengea heshima.
0 comments:
Post a Comment