TIMU za Barcelona na zitaendeleza upinzani wao wa muda mrefu kwenye michuano ya Ulaya baada ya kupangwa pamoja katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kikosi cha Antonio Conte kilizidiwa kete kileleni mwa Kundi C na Roma na sasa kitasafiri kwenda Nou Camp kwa mchezo wa mtoano.
Tottenham iliyovuna pointi nyingi zaidi kihistoria msimu huu, itamenyana na mabingwa wa Italia, Juventus, waliomaliza nyuma ya Barcelona kwenye Kundi D.
Vibara wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamepangiwa timu nafuu kidogo Basle, wakati Liverpool baada ya kuongoza Kundi E itamenyana na Porto.
Hii inakuwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2003-2004 timu tano kutoka nchi moja kuingia hatua ya mtoano.
Timu nyingine ya England katika hatua hii, Manchester United itamenyana na Sevilla ya Hispania kuwania tiketi ya Robo Fainali.
Katika droo iliyopangwa leo, mabingwa watetezi, Real Madrid watamenyana na Paris Saint-Germain.
Chelsea na Barcelona zimekutana mara 15 kwenye michuano ya Ulaya, kila timu ikishinda mechi tano na nyingine tano zimetoka sare.
Mechi za kwanza za 16b Bora zitachezwa Februari 13 na 14 na Februari 20 na 21, wakati marudiano yatakuwa Machi 6 na 7 na Machi 13 na 14.
0 comments:
Post a Comment