TIMU ya Arsenal itamenyana na Ostersunds ya Sweden inayomilikiwa na Muingereza, Graham Potter katika hatua ya 32 ya Europa League.
Atletico Madrid imepangwa na Copenhagen wakati Borussia Dortmund itamenyana na Atalanta, iliyoifunga Everton nyumbani na ugenini na kuongoza Kundi E.
Celtic itakuwa na safari ndefu hadi Urusi baada ya kikosi cha Brendan Rodgers kupangiwa Zenit St Petersburg ya Roberto Mancini.
Arsenal itamenyana na Ostersunds ya Sweden inayomilikiwa na Muingereza, Graham Potter katika hatua ya 32 ya Europa League PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Nayo Lyon, wenyeji wa fainali itakayopigwa Mei 16 mwakani, watamenyana na Villarreal na mchezo mwingine utazikutanisha Leipzig na Napoli.
Kocha Gennaro Gattuso wa AC Milan amepewa Ludugorets ya Bulgaria.
Mechi za kwanza zitachezewa Februari 15 na marudiano yatakuwa Februari 22, mwaka 2018.
0 comments:
Post a Comment