KOCHA Tony Pulis amefukuzwa West Brom Albion baada ya matokeo mabaya katika Ligi Kuu ya England.
Mmiliki, Guochuan Lai amechukua hatua hiyo baada ya kushuhudia timu yake ikichapwa mabao 4-0 na Chelsea mwishoni mwa wiki.
Kipigo cha juzi kilifanya mashabiki wa timu hiyo washinikize kuondolewa kwa kocha huyo wakibeba hadi mabango ya kutaka Pulis aondoke.
Tony Pulis amefukuzwa West Brom Albion baada ya kipigo cha 4-0 kutoka kwa Chelsea mwishoni mwa PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Pulis aliambiwa na Mwenyekiti, John Williams kwa simu leo asubuhi kwamba ameondolewa na West Brom itaanza kusaka kocha mpya.
Lai na Williams wamechukua hatua hiyo baada ya timu kushinda mechi mbili tu tangu kati ya 21 za Ligi Kuu ambayo inaiweka West Brom kwenye hatari ya kushuka dartaja.
Klabu huyo inabebwa na pointi moja tu kuangukia kwenye eneo la kushuka daraja ambako iko juu kwa nafasi moja tu.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59, ambaye alipata chakula cha jioni na Lai Ijumaa alisema: "Kitu kikubwa hii si juu ya Mwenyekitiu, wamiliki au mwingine yeyote. Ni kuhusu klabu ya soka na ni maamuzi sahihi kwa klabu ya soka,".
Alipoulizwa kama uamuzi sahihi ni kumpokonya majukumu yake, Pulis alisema: "Nimekuwa kwenye mchezo kwa muda mrefu wa kutosha kujua kwamba unapopata matokeo mabaya nini kitatokea,".
Msaidizi wa Pulis, Gary Megson anatarajiwa kukishikilia kikosi cha kwanza kwa muda kabla ya kupatikana kwa kocha mpya na atakiongoza kwenye mchezo dhidi ya Tottenham Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment