// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TASWA YATEUA KAMATI YA UCHAGUZI, MWENYEKITI WAMBURA WA BODI YA LIGI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TASWA YATEUA KAMATI YA UCHAGUZI, MWENYEKITI WAMBURA WA BODI YA LIGI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 24, 2017

    TASWA YATEUA KAMATI YA UCHAGUZI, MWENYEKITI WAMBURA WA BODI YA LIGI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), iliyokutana Dar es Salaam hivi karibuni, imeteua wanahabari tisa kuunda Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya chama. 
    Wengi wa walioteuliwa ni wanachama wa TASWA na wengine ni viongozi wa zamani wa chama na pia baadhi ni wanahabari wa michezo. 
    Mwenyekiti wa kamati hiyo atakuwa ni Mwenyekiti wa zamani wa TASWA, Boniface Wambura ambaye licha ya kuwa mwanahabari pia ana taaluma ya sheria na kwa sasa ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) na Katibu wa Kamati atakuwa Wakili Emmanuel Muga. 
    Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TASWA, Boniface Wambura ambaye pia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi  

    Wajumbe ni Katibu Mkuu wa zamani wa TASWA, Abdul Mohammed wa gazeti la Mwananchi, Mhazini Msaidizi wa zamani wa TASWA ambaye kwa sasa ni Mhariri wa michezo wa gazeti la Daily News, Nasongelya Kilyinga.
    Wajumbe wengine ni Florian Kaijage kutoka Azam Media,  Mahmoud Zubeiry kutoka Bin Zubeiry Sports - Online,  Tunu Hassan wa EFM Redio, Benny Kisaka wa Jambo Concept na Majuto Omary wa gazeti la Citizen.
    Hatua ya kuunda kamati hiyo inatokana na maelekezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ambalo limetaka chama kifanye marekebisho ya katiba  kwanza ili iwe rahisi kwa mambo mengine yafanyike katika utaratibu mzuri ikiwa ni pamoja na Uchaguzi Mkuu wa chama. 
    Kutokana na hali hiyo, Kamati ya Utendaji imekabidhi jukumu hilo kwa Kamati Maalum ambayo itapanga utaratibu wake wa namna ya kufanyia marekebisho katiba hiyo, ikimaliza itawasilisha rasimu ya Katiba kwenye Mkutano Mkuu wa chama kwa hatua nyingine. 
    Ni imani ya Kamati ya Utendaji kwamba Kamati ya Katiba inaweza kukamilisha rasimu hiyo katika muda usiozidi siku 90, ikiwa chini ya hapo itakuwa vizuri zaidi. 
    Tunaomba wadau wote tuipe ushirikiano wa namna mbalimbali kwa kadri itakavyowezekana ili tupige hatua katika kuimarisha chama chetu. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TASWA YATEUA KAMATI YA UCHAGUZI, MWENYEKITI WAMBURA WA BODI YA LIGI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top