// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); STARS KUANZA NA LIBYA KOMBE LA CHALLENGE, IPO KUNDI MOJA NA KENYA, RWANDA, ZANZIBAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE STARS KUANZA NA LIBYA KOMBE LA CHALLENGE, IPO KUNDI MOJA NA KENYA, RWANDA, ZANZIBAR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, November 16, 2017

    STARS KUANZA NA LIBYA KOMBE LA CHALLENGE, IPO KUNDI MOJA NA KENYA, RWANDA, ZANZIBAR

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi A katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge pamoja na ndugu zao, Zanzibar, wenyeji Kenya, Rwanda na waalikwa Libya.
    Katika droo iliyopangwa leo mjini Nairobi, Kenya ambako michuano hiyo inafanyika kuanzia Desemba 3 hadi 17, mwaka huu, Kundi B lina timu za Uganda, Zimbabwe, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.
    Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya Rwanda.
    Kilimanjaro Stars itafungua dimba na Libya Desemba 3, mwaka huu kwenye Kombe la CECAFA Challenge

    Kili Stars itarudi uwanjani Desemba 7 kumenyana na Zanzibar Heroes, Desemba 9  na Rwanda kabla ya kumaliza mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na wenyeji, Kenya Desemba 11.
    Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Desemba 12 na Nusu Fainali zitachezwa Desemba 14 na 15, wakati Desemba 16 itachezwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu ikifuatiwa na fainali.
    CECAFA Challenge ndiyo michuano mikongwe zaidi ya soka barani Afrika ambayo ilianza mwaka 1926 ikijulikana kama Kombe la Gossage hadi mwaka 1966, ilipobadilishwa na kuwa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati hadi mwaka 1971 ilipobadilishwa tena na kuwa CECAFA Challenge.
    Wadhamini tofauti wamekuwa wakiingia na kutoka kwa kipindi chote hicho, lakini taarifa zinasema kuanzia mwaka huu Televisheni namba moja Afrika Mashariki na Kati, Azam TV ndiyo wanakuwa wadhamini wapya ambao pia watakuwa wanarusha moja kwa moja michuano hiyo. 
    Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na Tanzania mara tatu.
    Uganda, The Cranes pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.  

    RATIBA CHALENGE 2017
    Desemba 3, 2017
    Libya vs Tanzania
    Kenya vs Rwanda
    Desemba 4, 2017
    Burundi vs Ethiopia
    Uganda vs Zimbabwe
    Desemba 5, 2017
    Zanzibar vs Rwanda
    Kenya vs Libya
    Desemba 6, 2017
    Sudan Kusini vs Zimbabwe
    Uganda vs Burundi
    Desemba 7, 2017
    Tanzania vs Zanzibar
    Rwanda vs Libya
    Desemba 8, 2017
    Sudan Kusini vs Ethiopia
    Zimbabwe vs Burundi
    Desemba 9, 2017
    Rwanda vs Tanzania
    Kenya vs Zanzibar
    Desemba 10, 2017
    Sudan Kusini vs Burundi
    Ethiopia vs Uganda
    Desemba 11, 2017
    Libya vs Zanzibar
    Kenya vs Tanzania
    Desemba 12, 2017
    Uganda vs Sudan Kusini
    Zimbabwe vs Ethiopia
    Desemba 13, 2017
    MAPUMZIKO
    Desemba 14, 2017
    NUSU FAINALI
    Mshindi Kundi A Vs Mshindi wa Pili Kundi B
    Desemba 15, 2017
    Mshindi Kundi B Vs Mshindi wa Pili Kundi A
    Desemba 16, 2017
    MAPUMZIKO
    Desemba 17, 2017
    Fainali/Mshindi wa Tatu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS KUANZA NA LIBYA KOMBE LA CHALLENGE, IPO KUNDI MOJA NA KENYA, RWANDA, ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top