// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KESHO SUMBAWANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KESHO SUMBAWANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 10, 2017

    SIMBA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KESHO SUMBAWANGA

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    BAADA ya sare ya 0-0 na Nyundo FC jana Uwanja wa Azimio, Mpanda mkoani Katavi Jumanne, Simba SC inatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa kirafiki kesho Sumbawanga.  
    Nyundo FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara, Jumanne iliwafurahisha mashabiki wa nyumbani kwenye Uwanja wa Azimio kwa soka safi na kuwabana vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sare ya 0-0.
    Kocha Mcameroon, Joseph Omog aliridhishwa na viwango vya wachezaji ambao wamekuwa hawapati nafasi mara kwa mara kikosini, baada ya wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza kwenda kwenye timu zao za taifa.  
    Ally Shomary ni kati ya wachezaji walio na kikosi cha Simba Sumbawanga

    Lakini kilikuwa kikosi imara kikiundwa na viungo mahiri, Mwinyi Kazimoto, Muzamil Yassin, Mohammed Ibrahim na washambuliaji, Mrundi Laudit Mavugo na Mghana, Nicholas Gyan ambacho kilishindwa kuonyesha cheche kwenye Uwanja wa uzio wa fito.   
    Na sasa kikosi kipo Sumbawanga tangu juzi ambako kesho kitakuwa na mechi nyingine ya kirafiki, kabla ya Jumapili kurejea Mbeya kuendelea na maandalizi ya mchezo wake ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Tanzania Prisons Novemba 18 Uwanja wa Sokoine.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KESHO SUMBAWANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top