MKURUGENZI wa Ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo amehitimisha miaka yake 10 ya kufanya kazi katika klabu hiyo kwa kujiuzulu na kuondoka huku pia mustakabali wa kocha Antonio Conte ukiwa shakani.
Habari zinasema mtaalamu huyo mwenye umri wa miaka 52, ambaye anaweza kujiunga na Monaco, kuondoka kwake katika klabu hiyo ni pigo kwa mmiliki, Roman Abramovich.
Abramovich amekuwa akimtumia Mnigeria huyo kama mtu muhimu katika bodi yake kwenye klabu hiyo ya Magharibi mwa London - akiwa miongoni mwa watu wachache ambao Mrusi huyo anawaamini na kufuata ushauri wao.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo amehitimisha miaka yake 10 ya kufanya kazi Stamford Bridge PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Huu umekuwa uamuzi mgumu kuufanya, lakini ni ambao naamini ni sahihi kwa wote, kwangu na familia yangu na klabu," alisema Emenalo katika taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya klabu.
"Nimekuwa na kipaumbele cha kufanya kazi na watu wenye vipaji mno katika ulimwengu wa michezo kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita, na nitaondoka huku nikijivunia amafanikio tuliyoyapata,".
"Naitakia Chelsea kila mafanikio na isonge mbele na kuwa na mustakabali mzuri zaidi,".
Kuondoka kwa Emenalo kumemuachia masikitiko makubwa kocha Conte ambaye alisema;
"Ninampa pole sana Michael kuondoka Chelsea, na ningependa kumshukuru kwa msaada wake wote na sapoti aliyonipa tangu nawasili katika klabu hii,".
The Blues imetwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, Kombe la FA, Kombe la Ligi, Europa League na Ligi ya mabingwa wakati Emenalo alipokuwa katika klabu hiyo.
Taji la mwisho la ubingwa wa Ligi Kuu England Chelsea imetwaa chini ya kocha wa sasa, Conte katika msimu wake wa kwanza kwenye soka ya Uingereza. Pamoja na hayo, Mtaliano huyo amejikuta katika msimu mgumu wa pili hadi sasa.
Michael Emenalo (katika picha iliyozungushiwa duara) nyuma ya Antonio Conte katika ushindi wa Chelsea wa 1-0 dhidi ya Manchester United Uwanja wa Stamford Bridge jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Emenalo aliishuhudia Chelsea ikiwapiga wapinzani wao katika mbio za ubingwa, Manchester United 1-0 Uwanja wa Stamford Bridge jana.
Ushindi huo Magharibi mwa London Jumapili ulipatikana bila beki Mbrazil, David Luiz kuwemo kikosini ambaye alienguliwa kwenye kikosi baada ya kutifatiana na Conte.
Ugomvi wa sasa wa Conte na Luiz ni mwendelezo wa matatizo yake na wachezaji, ambavyo vinamuweka shakani kuendelea na kazi Stamford Bridge
Awali aligombana na mshambuliaji Diego Costa na kiungo Nemanja Matic, ambao wote wameondoka kwenye klabu hiyo.
Awali aligombana na mshambuliaji Diego Costa na kiungo Nemanja Matic, ambao wote wameondoka kwenye klabu hiyo.
Kocha huyo alisem akweamba Mbrazil huyo anaweza kupata nafasi ya kucheza iwapo tu atajifunza namna ya kukaa na wachezaji wake.
"(Andreas) Christensen ana umri wa miaka 22 tu, ameonyesha haiba nzuri, kwa hakika yupo na ataendelea kuwapo Chelsea, sawa na Ethan Ampadu.
"David Luiz anatakiwa kufanya kazi na watu wengine pia kama dhamira yake ni kucheza, vinginevyo atabaki jukwani au benchi,".
Conte alikuwas kocha wa 10 kuteuliwa Chelsea chini ya Emenalo Magharibi mwa London na amekuwa akishutumiwa kwa usajilo alioufanya majira haya.
Kocha huyo wa zamano wa Juventus ameshindwa kuifanya Chelsea itoshe licha ya kuwezeshwa kuwasajili wachezaji wapya kama Alvaro Morata, Antonio Rudiger, Tiemoue Bakayoko, Danny Drinkwater, Davide Zappacosta na Willy Caballero.
Na haya yanajirudia, baada ya msimu wake wa kwanza kuondoka kwa Nemanja Matic na Costa - ingawa baadaye uhusiano wake na wachezaji ulifanyiwa marekebisho.
Emenalo alijiunga na Chelsea kwa mara ya kwanza chini ya Myahudi, Avram Grant mwaka 2007 kabla ya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi miaka minne baadaye. Amekuwa muhusika mkuu wa usajili wa wachezaji na mtaalmu wa mtandao wa kuskauti wachezaji vijana Celsea.
0 comments:
Post a Comment