KLABU ya Barcelona imekubali kumpa mkataba mpya nyota wake, Lionel Messi hadi mwaka 2021 na sasa wanajiandaa kumpa mkataba wa maisha, kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania.
Mkataba wa Messi ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu, maana yake angekuwa huru kuanza mazungumzo na klabu nyingine za Ulaya mwezi Januari.
Lakini Rais wa La Liga, Javier Tebas ametangaza wiki hii kwamba Messi amesaini mkataba mpya wa miaka minne na kumaliza tetesi zinazohusu mustakabali wake.
Gazeti la Mundo Deportivo lina habari inayosema 'Messi wa masha' Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Gazeti la Mundo Deportivo limeripoti kwamba mkataba mpya ulisainiwa tangu Juni na sasa Barcelona imeanza mchakato wa kumsainisha mkataba utakaomfanya abaki Nou Camp 'maisha'.
Mshindi huyo wa Ballon d'Or mara tano ameanza vizuri msimu huu akifunga mabao 12 katika mechi 11 za La Liga na kuiweka Barcelona kileleni, wakiwazidi pointi nne Valencia walio nafasi ya pili na pointi nane kwa zaidi ya mahasimu wao, Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment