Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kwa mchezo mmoja kufanyika kesho Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, ambako mwenyeji Maji Maji FC wataikaribisha Stand United ya Shinyanga.
Ligi Kuu itaendelea tena Jumamosi kwa michezo mingine mitano kuchezwa kwenye viwanja tofauti, kama wa kesho na hiyo itaanza Saa 10:00 jioni.
Michezo hiyo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Singida United itakayocheza na Yanga SC kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida wakati Tanzania Prisons itakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Njombe Mji kwa upande wake watakuwa wenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe huku Mtibwa Sugar ikisafiri kutoka Morogoro kwenda Mtwara kucheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Hizo ni mechi zitakazochezwa saa 10.00 jioni.
Mchezo pekee utakaofanyika saa 1.00 usiku utakuwa ni kati ya Azam FC na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam.
Jumapili kutakuwa na michezo miwili ya Ligi Kuu ambako Lipuli ya Iringa itakuwa mwenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Samora wakati Simba itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi hizo zitaanza saa 10.00 jioni.
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kwa mchezo mmoja kufanyika kesho Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, ambako mwenyeji Maji Maji FC wataikaribisha Stand United ya Shinyanga.
Ligi Kuu itaendelea tena Jumamosi kwa michezo mingine mitano kuchezwa kwenye viwanja tofauti, kama wa kesho na hiyo itaanza Saa 10:00 jioni.
Michezo hiyo ya Jumamosi itakuwa ni kati ya Singida United itakayocheza na Yanga SC kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida wakati Tanzania Prisons itakuwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera.
Wachezaji tegemeo wa Maji Maji, Danny Mrwanda na Jerry Tegete (kushoto) |
Mchezo pekee utakaofanyika saa 1.00 usiku utakuwa ni kati ya Azam FC na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam.
Jumapili kutakuwa na michezo miwili ya Ligi Kuu ambako Lipuli ya Iringa itakuwa mwenyeji wa Mwadui FC ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Samora wakati Simba itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi hizo zitaanza saa 10.00 jioni.
0 comments:
Post a Comment