Na Mwandishi Wetu, MILAN
ITALIA, moja ya mataifa makubwa kisoka itakosekana kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwakani kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50.
Hiyo ni kufuatia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Sweden usiku wa jana Uwanja wa San Siro, Milan katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania tiketi ya Urusi 2018.
The Azzurri wanaishia hapa baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza nchini Sweden, kikosi cha Gian Piero Ventura kikizikosa fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.
Shujaa wa Sweden ni Jakob Johansson aliyefunga bao pekee kwenye mchezo wa kwanza na kumkosesha fainali za sita za Kombe la Dunia kipa Gianluigi Buffon, ambaye jana aliichezea kwa mara ya mwisho Italia katika mechi ya 175.
Kipa Gianluigi Buffon akipunga mkono kuaga kwa huzuni baada ya Italia kuzikosa fainali za Kombe la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
“Si pole kwangu tu, bali kwa soka nzima ya Italia,”amesema kipa huyo mwenye umri wa miaka 39, Buffon, aliyetunguliwa na Jakob Johansson kwenye mechi ya kwanza mjini Stockholm Ijumaa na hilo limekuwa bao pekee la kujivunia kwa Sweden.
“Tumekwama katika kitu fulani, ambacho pia kinamaanisha kitu fulani katika ujamaa. Inasikitisha kumaliza namna hii. Lawama ni za wote baina yetu. Hakuna wa kumfanya mbuzi wa kafara. Kushinda pamoja, kufungwa pamoja,”alisema.
“Ninaondoka timu ya Italia kwa huzuni. Kumkumbatia kila mmoja, hususan wale ambao tumekuwa wote katika safari hii ya kipekee,”aliongeza kwa machungu huku machozi yakimtoka,”.
Buffon, mshindi wa Kombe la Dunia mwaka 2006, anafahamu Italia huungana kama nchi The Azzurri inapofanya vizuri. Wameshinda Kombe la Dunia mara nne na mara mbili wamefungwa kwenye fainali.
Picha za Toto Schillaci, Roberto Baggio, Luigi Riva, Marco Tardelli na Dino Zoff zinaambatana na historia ya mafanikio hayo.
Italia walimaliza nafasi ya pili katika Kundi, ambalo Hispania iliongoza kabla ya kushindwa kufunga ndani ya dakika 180 dhidi ya Sweden.
Italia; Buffon, Barzagli, Bonucci, Chiellini, Candreva, Florenzi, Jorginho, Parolo, Darmian/El Shaarawy dk64, Immobile, Gabbiadini/Belotti dk64.
Sweden; Olsen, Lustig, Lindelhof, Grandqvist, Augustinsson, Claesson/Rohden dk72, Johansson/Svensson dk19, Larsson, Forsberg, Toivonen/Kiese Thelin dk54 na Berg.

0 comments:
Post a Comment