Eric Dier atakuwa mchezaji wa sita kuvaa beji ya Unahodha wa timu ya taifa ya England chini ya kocha Gareth Southgate leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA
NYOTA wa Tottenham Hotspur, Eric Dier atakuwa Nahodha wa sita wa England chini ya kocha
Gareth Southgate wakati atakapouiongoza timu yake ya taifa dhidi ya Ujerumani kwenye mchezo wa kirafiki leo.
Huku Manodha wote wawili wa timu, Harry Kane na Jordan Henderson wakiwa nje kwa sababu ya majeruhi, Gary Cahill anasumbuliwa na maumivu ya mgongo na Joe Hart anatarajiwa kuanzia benchi, hivyo Dier atakuwa Nahodha wa England Uwanja wa Wembley Ijumaa.
Huyo atakuwa mchezaji wa sita kuvaa kitambaa cha Unahodha wa timu ya taifa tangu Southgate achukue nafasi ya Sam Allardyce mwaka jana.
Kane, Henderson, Cahill, Hart na Wayne Rooney wote wamekwishakuwa Manahodha wa England chini ya Southgate.
0 comments:
Post a Comment