MCHEZAJI anayetakiwa na Barcelona, Philippe Coutinho ataiomba Liverpool ikatae ofa yoyote itakayotolewa na Paris Saint-Germain kwa sababu ni yake ni kuhamia Nou Camp.
Kiungo huyo Mbrazil alikuwa mchezaji anayetakiwa mno na vigogo wa Katalunya, ambao waliwajaribu Wekundu hao kwa dau la Pauni Milioni 114 Agosti mwaka huu.
Liverpool ilisistiza kwamba Coutinho alikuwa hauzwi, lakini klabu ya Hispania ikarudi na dau la Pauni Milioni 106 mwezi Januari.
Kwa mujibu wa gazeti la Sport, Paris Saint-Germain pia ilikuwa inajiandaa kupeleka maombi ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Philippe Coutinho ameiomba Liverpool ikatae ofa yoyote itakayotolewa na Paris Saint-Germain PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Vigogo wa Ligue 1 wana imani watafanikiwa kumshawishi Mbrazil huyo ambaye ni mwaka jana tu alisaini mkataba mpya Anfield, akubali kuhamia Jiji la Ufaransa badala ya Nou Camp.
Lakini gazeti la Hispania limeandika kwamba Coutinho hameiomba Liverpool kutomuuza PSG. "Ameowataka wawakilishi wake kupuuza ofa yoyote kutoka kwao. Mojawapo ni ya PSG," wamesema.
0 comments:
Post a Comment