KIPA mkongwe wa Juventus, Gianluigi Buffon ameongeza tuzo baada ya kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa wa Msimu uliopita wa Serie A katika sherehe za Gran Gala del Calcio.
Gwiji huyo wa Italia ameshinda tuzo hiyo baada ya kazi yake nzuri msimu wa 2016-17 katika sherehe zilizofanyika mjini Milan usiku wa jana zikiandaliwa na Shirikisho la Soka Italia.
Na ulikuwa usiku mwingine mzuri kwa kwa kikosi cha Massimiliano Allegri cha Juventus ambacho kilitawala katika tuzo za Serie A ukumbi wa Megawatt Court.
Gianluigi Buffon akiwa ameshika tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Serie A msimu wa 2016-17 usiku wa jana katika Gran Gala del Calcio PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Wachezaji saba wa Juventus wameingia kwenye kikosi Bora cha Serie A cha msimu 2016-17, wakiwemo Buffon, Dani Alves, Leonardo Bonucci, Alex Sandro, Miralem Pjanic, Gonzalo Higuain na Paulo Dybala.
Wengine wanne ni Kalidou Koulibaly, Radja Nainggolan, Marek Hamsik na Dries Mertens.
Zaidi ya hayo, Kibibi Kizee cha Turin opia kimebeba tuzo ya Klabu Bora ya Msimu kwa mara ya sita mfululizo, siku moja tu baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Crotone katika Serie A.
Juventus kwa sasa wanashika nafasi ya tatu katika katika ligi hiyo kubwa zaidi Italia, wakizidiwa pointi nne na vinara, Napoli baada ya mechi zao 14 za awali.
Na timu hizo mbili zinatarajiwa kukutana Ijumaa katika mchezo mkali Uwanja wa San Paolo, huku Juventus wakitarajiwa kupunguza idadi ya pointi wanazozidiwa.
Na mchezo wao utakaofuata wa Serie A hautakuwa mwepesi pia, kwani watamenyana na Inter Milan, wanaoshika nafasi ya pili wakiizidi pointi mbili Juventus.
0 comments:
Post a Comment