// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AUBAMEYANG 'ASIMAMISHWA' BORUSSIA DORTMUND BAADA YA KWENDA KUJIRUSHA BARCELONA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AUBAMEYANG 'ASIMAMISHWA' BORUSSIA DORTMUND BAADA YA KWENDA KUJIRUSHA BARCELONA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, November 17, 2017

    AUBAMEYANG 'ASIMAMISHWA' BORUSSIA DORTMUND BAADA YA KWENDA KUJIRUSHA BARCELONA

    MSHAMBULIAJI Pierre-Emerick Aubameyang hajajumuishwa kwenye kikosi cha Borussia Dortmund kitakachomenyana na Stuttgart kwa sababu za kinidhamu. 
    Dortmund imesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kujibu swali la shabiki, ambaye aliuliza kwa nini Aubameyang hakuwemo kwenye video ya kikosi kilichowasili Uwanja wa Ndege.
    Timu hiyo ya Bundesliga ikajibu: "Aubameyang ameondolewa kwenye kikosi cha mechi ya kesho kwa sababu za kinidhamu,".
    Gazeti la Bild la Ujerumani limeripoti kswamba Aubameyang alitumia siku zake mbili za mapumziko kupisha mechi za kimataifa kwenda Barcelona.  

    Pierre-Emerick Aubameyang 'amesimamishwa' Borussia-Dortmund baada ya kwenda kustarehe Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA 

    Aubameyang alimtembelea mchezaji mwenzake wa zamani wa Ousmane Dembele na akaenda katika klabu ya usiku mjini Barcelona, Shoko na kaka yake Willy katika safari hiyo. 
    Mshambuliaji huyo akaposti picha yake Instagram akiwa na Dembele, ambaye alicheza naye msimu uliopita Dortmund.
    Aubameyang ameingia kwenye matatizo na Dortmund hivi karibuni. Aliachwa kwenye kikosi cha Dortmund kilichomenyana na Sporting Lisbon msimu uliopita baada ya kutumia siku yake mapumziko kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa ya rafiki wake mjini Milan kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa.
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, kwa mara nyingine amekuwa na mwanzo mzuri wa msimu, akifunga mabao 15 katika mechi 12 zikiwemo hat-tricks mbili za Bundesliga. 
    Lakini baada ya hapo mabao yakakauka kwa mshambuliaji huyo ambaye amefikisha dakika 476 bila kutikiswa nyavu baada ya kutofunga pia timu hiyo ikifungwa 3-1 na Bayern Munich mara ya mwisho.
    Aubameyang amefunga mabao 31 katika mechi 32 za Bundesliga alizocheza msimu uliopita, baada ya kuanza kucheza pamoja na Dembele kwenye safu ya ushambuliaji.  
    Dembele alihamia Barcelona msimu huu kw aada ya uhamisho ya Pauni Milioni 96 kwenda kuziba pengo la Neymar, lakini ombi la Aubameyang kwenda timu ya Ligi Kuu ya China halijafanyiwa kazi na ameendelea kubaki Signal Iduna Park.  
    Dortmund itamenyana na Stuttgart leo usiku kutafuta ushindi wao wa kwanza kwenye Bundesliga tangu Septemba 30, walipoifunga 2-1 Augsburg.
    Baada ya hapo, vigogo hao wa Ujerumani watahamia Ulaya, ambako wataikaribisha Tottenham kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa usiku wa Jumanne.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AUBAMEYANG 'ASIMAMISHWA' BORUSSIA DORTMUND BAADA YA KWENDA KUJIRUSHA BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top