MSHAMBULIAJI Sergio Aguero amezua hofu Manchester City baada ya kuzimia wakati wa mapumziko kwenye mchezo wa kirafiki Argentina ikifunga na Nigeria.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alifunga bao moja timu yake ikichapwa 4-2 Uwanja wa Krasnodar nchini Urusi, lakini akashindwa kurudi kipindi cha pili.
Aguero, ambaye amepona maumivu ya mbavu aliyoyapata katika ajali ya gari nchini Uholanzi na ameanza mazoezi mwezi huu alizimia kwenye chumba cha kubadilishia nguo na kukimbizwa hospitali.
City, ambayo itamenyana na Leicester Jumamosi, inasubiri taarifa za madaktari kabla ya mshambuliaji huyo kurejea nyumbani.Sergio Aguero akicheza dhidi ya Nigeria Uwanja wa Krasnodar kabla ya kuzimia wakati wa mapumziko PICHA ZAIDI GONGA HAPA
0 comments:
Post a Comment