UHUSIANO wa Gerard Pique na Sergio Ramos umevunjika rasmi, na ni baada ya taarifa ya beki wa Barcelona kuripotiwa kuleta matatizo katika kambi ya timu ya taifa ya Hispania.
Pique alizomewa na mashabiki wa Hispania katika siku ya kwanza ya mazoezi mjini Madrid Jumatatu kuelekea mechi za timu za kufuzu Kombe la Dunia.
Nyota huyo wa Barca amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa tamko la kuunga watu wa Katalunya kupewa uhuru na kujitenga kutoka Hispania.
Ametwaa mataji ya Kombe la Dunia na Euros akiwa na Hispania mwaka 2010 na 2012, lakini mipigia debe mpango wa Katalunya kupewa Uhuru wajitenge.
Uhusiano wa mabeki wa kati wa Hispania, Gerard Pique na Sergio Ramos umevunjika rasmi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Kwa mujibu wa gazeti la AS matatizo yanaongezeka kwa beki huyo kutokana na kuvunjika kwa mahusiano yake pacha wake wa muda mrefu katika beki ya kati ya Hispania, Ramos.
Nahodha wa Hispania, Ramos alimshutumu mchezaji mwenzake wa zamani, Pique wiki iliyopita kwa kutoa kauli ya kuungano Katalunya kupewa Uhuru na kujitenga.
Ramos na Pique wamekuwa alama ya upinzani wa Real Madrid na Barcelona na pia wamekuwa wakicheza kwa pamoja kwa muda mrefu katika beki ya kati ya Hispania.
Lakini sasa inaelekea mwisho wao wa kucheza pamoja umewadia kutoka na shinikizo la Pique kuondolewa kwenye kikosi cha Hispania.
Pique amesema hana tatizo kutochezea Hispania ikiamuliwa hivyo na Julen Lopetegui na Chama cha Soka cha Hispania kwamba yeye ni tatizo katika mgogoro wa kisiasa unaendelea nchini.
Alizomewa wakati wa mazoezi ya timu ya taifa juzi huku mashabiki wakimtaka Pique aondoke kwenye kambi ya mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Albania na Israel.
Kulikuwa kuna mashabiki wapatao 1,500 walioruhusiwa kutazama mazoezi ya timu waliokuwa wanaimba 'Pique carbon, Espana es tu nacion' ambayo ina maana 'Pique mwanaharamu Hispania ni taifa lako'.
Bango moja lilikuwa limeandikwa, Kikatalunya, likisomeka; 'Pique nje' na lingine lilisomeka: 'Mama yangu amesema kuwa huru, unatakiwa kuondoka nyumbani.' El Mundo Deportivo limeripoti kwamba Polisi wa Hispania waliondoa bango moja lililokuwa linasomeka: 'Pique hatutaki uondoke; tunataka ufukuzwe. Umechukiza,".
0 comments:
Post a Comment