KOCHA Craig Shakespeare amefukuzwa Leicester City miezi minne tu tangu arithi mikoba ya Claudio Ranieri.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 aliitwa kwenye kikao na uongozi wa juu leo kutaarifiwa juu ya uamuzi wa kufukuzwa kwake baada ya kuiongoza timu kushinda mechi moja tu kati ya 10 za Ligi Kuu ya England na kuwafanya mabingwa hao wa msimu wa 2015-2016 washike nafasi ya 18 sasa kwenye msimamo.
The Foxes walilazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 nyumbani na West Brom jana usiku usiku na wameshinda mechi tatu tu msimu huu, mechi mbili wakishinda kwenye Kombe la Carabao.
Shakespeare alichukua nafasi ya Ranieri mwezi Juni tu, akisaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kuiongoza vizuri timu hiyo kama kocha wa muda.
Craig Shakespeare amefukuzwa Leicester City miezi minne tu tangu arithi mikoba ya Claudio Ranier PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Aliiwezesha pia The Foxes kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kurithi mikoba ya Mtaliano huyo aliyefukuzwa Februari.
Shakespeare alipewa fedha nyingi za kutumia kusajili na akawachukua nyota kama Harry Maguire kwa Pauni Milioni 17 na Kelechi Iheanacho kwa Pauni Milioni 25.
Pamoja na hayo, Leicester imekuwa na matokeo mabaya msimu huu, ushindi wao pekee kwenye Ligi ukitoka kwa Brighton mwezi Agost.
Shakespeare hakutarajiwa kufukuzwa mapema kiais hiki, lakini wamiliki wa klabu hiyo kutoka Thailand waliamua kuchukua hatua baada ya kumuona Riyad Mahrez akifunga bao la kusawazidha dakika za mwishoni jana dhidi ya Baggies.
0 comments:
Post a Comment