TIMU ya taifa ya Nigeria imefuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Zambia katika mchezo wa Kundi B jana Uwanja wa Akwa Ibom mjini Uyo.
Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee linaloipeleka Nigeria Urusi mwakani, winga wa Arsenal, Alex Iwobi aliyewainua vitini mashabiki wa Super Eagles dakika ya 73 baada ya nyota wa Chelsea, Victor Moses kushirikiana vizuri na Abdullahi Shehu kumsetia mfungaji kumaliza kazi.
Tunisia nayo imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Guinea kwenye mchezo wa Kundi A, huku Youssef Msakni akipiga hat-trick na Mohamed Ben Amor akifunga lingine.
Kocha wa Super Eagles, Gernot Rohr akirushwa juu na wachezaji wake baada ya ushindi wa jana dhidi ya Zambia na kufuzu Kombe la Dunia PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Naby Keita aliwafungia Guinea dakika ya 35 kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya mwisho.
Tunisia inaongoza Kundi hilo kwa pointi tatu zaidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walioshinda 2-1 dhidi ya Libya jana kuelekea mechi za mwisho.
Misri wanaweza kuwa timu nyingine kujihakikishia tiketi mapema kama wataifunga Kongo leo baada ya jana Uganda kulazimishwa sare ya 0-0 na Ghana katika mchezo wa Kundi E mjini Kampala.
0 comments:
Post a Comment