MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Neymar amefungiwa mechi moja baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Marseille.
Sasa Mbrazil huyo ataukosa mchezo wa leo wa Ligue 1 Ufaransa dhidi ya Nice. Pamoja na hayo, Neymar ataadhibiwa zaidi akirudia kosa.
Dhidi ya Marseille, mshambuliaji huyo alikasirika baada ya kuchezewa rafu na Lucas Ocampos dakika ya 87 na kumsukuma hado chini winga huyo wa Argentina.
Matokeo yake yakawa ni kuonyeshwa kadi ya pili ya njano hivyo mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 198 PSG kutoka Barcelona, akatolewa kwa kadi nyekundu.
Neymar atakosekana kwenye mchezo wa leo dhidi ya Nice akitumikia adhabu ya kadi PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Japokuwa kikosi cha Unai Emery kitamkosa mchezaji wake huyo ghali leo, lakini hapana shaka Edinson Cavani na Kylian Mbappe watatosha kuisaidia PSG kushinda.
0 comments:
Post a Comment