KIUNGO Mjerumani wa Arsenal, Mesut Ozil ghafla anatakiwa na mahasimu, Manchester United.
Kiungo huyo wa The Gunners yupo kwenye mikakati ya kocha Mreno, Jose Mourinho katika dirisha dogo Januari atakapokuwa huru baada ya kumaliza mkataba wake Emirates.
Lakini inaonekana Old Trafford hawajaridhishwa na mpango wa kusajiliwa kwa Ozil, zaidi hawavutiwi na uchezaji wake na hata mshahara atakaotaka akikubali kuhama.
Mourinho alifanya kazi na Ozil katika klabu ya Real Madrid na anajiamini anaweza kumshawsihi kuhama Kaskazini Magharibi.
Wawili hao wote waliingia klabu ya Santiago Bernabeu mwaka 2010 na kujenga uhusiano mzuri, kwani Ozil alikuwa anaaminiwa mno Mourinho walipokuwa Hispania.
Na kocha huyo Mreno hivi karibuni aliandika maelekezo kwenye autobiography ya Ozil.
Ozil ameruhusu mkataba wake ufike mwisho Arsenal na hakuna hata dalili za mazungumzo ya mkataba mpya.
Mchezaji mwenye umri wa miaka 28, anataka kulipwa zaidi ya Pauni 300,000 kwa wiki ili kusaini mkataba mpya Arsenal.
Na hiyo ni kwa sababu pia Arsenal imeshinda mechi nne kati ya tano ambazo ilicheza bila Ozil ambaye yuko nje maumivu ya goti.
Inter Milan ya Italia ni timu nyingine inayomtaka mchezaji huyo. Ikumbukwe Man United pia walitoa ofa ya kumnunua Ozil wakati anaondoka Madrid mwezi Septemba mwaka 2013, lakini akaruhusiwa kujiunga na Arsenal.
0 comments:
Post a Comment