KOCHA wa Ubelgiji, Roberto Martinez amethibitisha Marouane Fellaini ameumia goti katika ushindi wa 4-3 wa timu yake dhidi ya wenyeji, Bosnia-Herzegovina Jumamosi.
Mchezaji huyo wa Manchester United sasa anatarajiwa kukosekana kwa wiki mbili kutokana na maumivu hayo ya goti lake la kulia, maana yake ataukosa mchezo dhidi ya Liverpool Jumamosi wakati ambao tayari Mashetani hao Wekundu wanawakosa Paul Pogba na Michael Carrick.
Pamoja na mchezo huo wa Anfield, Fellaini anatarajiwa kukosekana pia katika mechi dhidi ya Benfica kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Huddersfield kwenye Ligi Kuu England na Swansea kwenye Kombe la Carabao.
Martinez pia amethibitisha mshambuliaji wa Manchester United, Romelu Lukaku yuko fiti kuichezea Ubelgiji mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cyprus Jumanne baada ya kupona maumivu ya enka.
0 comments:
Post a Comment